Chin Bees Awadhihaki Wanaofanya Muziki wa Trap

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Licha ya wakali wote wanaofanya muziki wa Trap Bongo kama Country Boy, Moni Centrozone, Young Lunya na wengineo lakini bado Chin Bees amesema kwa sasa bado hajaona msanii anayefanya muziki huo labda watokee wasanii wengine.


Akizungumza hayo kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV Chin Bees amesema "Mpaka sasa sijasikia mtu anafanya Trap ila naona watu wanarap, labda wakitokea wasanii wapya lakini kwa sasa sioni mtu anayefanya muziki wa Trap"


"Kila kazi yangu ninayoitoa mimi inashika namba moja kuanzia kwenye Nesanesa, Nasebenza, Nyonga nyonga nimeanza zamani na sasahivi nina kampuni yangu ya BGE ndiyo maana kazi zangu za sasa ni tofauti na zamani".


Aidha Chin Bees ambaye anajiita mfalme wa muziki huo 'King Of Trap' amesema ameamua kuachana na lebo yake ya zamani kwa sababu anataka kusimama mwenyewe.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad