Dk. Gwajima Aridhishwa Uzalishaji Dawa Kiwanda cha Keko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima, ameridhishwa na uzalishaji wa dawa katika kiwanda cha dawa cha Keko Pharmaceutical na kusema kuwa kiwanda hicho kimeanza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

 

Amesema hayo baada ya kufanya ziara kiwandani hapo mapema leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi kwenye Bohari ya Dawa (MSD) na kutembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho na kuona jinsi uzalishaji wa dawa unavyoendelea huku katika kipindi cha miezi miwili (Oktoba mpaka Disemba) kikiwa kimetengeneza vidonge vya Paracetamol Milioni 25.

 

“Pamoja na kuwa kwamba MSD mlikuwa na majukumu matatu, kununua, kutunza na kusambaza lakini kwa kujibu maelekezo ya Serikali na mahitaji ya sasa mmeamua kufanya masuala ya uzalishaji, mmeweza kusimamia na kuhakikisha hisa za Serikali zimeongezeka kwenye kiwanda kwa asilimia 70 ambapo sasa mnazalisha vidonge vya Paracetamol Milioni 25 kwa miezi miwili.

 

“Haya nd’o maendeleo ambayo mnatakiwa taasisi kujiongeza kufuata mwelekeo wa nchi,”alisema waziri huyo.

 

Aidha,  amesema idadi hiyo ya vidonge inayozalishwa imeokoa fedha za Serikali kwa kiasi kikubwa ambapo kama vingeagizwa nje ya nchi Serikali ingetumia gharama kubwa.

 

Amewataka wakuu wa taasisi kujiongeza ili waende na mahitaji ya sasa kwa kutekeleza majukumu yake lakini pia waende na mwelekeo wa nchi na kujibu changamoto za kiuchumi duniani pamoja na changamoto za ongezeko la magonjwa ili yaweze kudhibitiwa na kutibiwa.

 

“Nimefarijika sana na serikali ipo pamoja na nyie, sio MSD pekee bali hata taasisi nyingine zote ambazo zina uwezo wa kuzalisha kitu fulani ndani ya taaluma na miundombinu yake,” ameongeza.

 

Pamoja na hayo, amefanya kikao na Menejimenti ya MSD ili kupata changamoto mbalimbali zinazowakabili na kupata muafaka wa pamoja.

Na Emmanuel Malegi-DSM

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad