Gigy Money Awaombea Msaada Amber Rutty na mumewe

 


Msanii Gigy Money amewaomba watu wa jamhuri ya mtandao wa Instagram kuchangia japo shilingi elfu 1 'bukubuku' kwa kila mmoja kwani inatosha kulipa faini ya kumtoa msanii Amber Rutty na mumewe ambao wapo nyuma ya nondo kwa sasa.

Gigy Money ameongea hilo baada ya kwenda Live kupitia ukurasa wake wa mtandao huo ambapo amesema kuwa 


"Nimem-miss Amber Rutty hivi ndiyo atolewi tena, miaka mitano jamani tuchangeni Instagram tucheke tukichanga bukubuku tunamtoa Amber Rutty atakuwa ameshajifunza jamani, tuchangeni tuwatoe wale" 


Siku ya Ijumaa Septemba 25, 2020 Amber Rutty pamoja na mumewe Saidi Bakary wamelikumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani kwa makosa manne ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments