Haji Manara Anatarajia Kufunga ndoa na Mchumba Wake leo

 


 Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, mapema jana amethibitisha kuwa ifikapo siku ya leo Alhamisi, tarehe 10, anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake aliyemtambulisha kwa jina Naheeda.

Haji amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba ndoa hiyo itafungwa katika msikiti wa Maamur na sherehe zitaendelea hapa hapa jijini hadi siku ya Jumamosi.


“Watu wangu wa nguvu karibuni katika harusi yangu itakayofungwa kesho Masjid Maamur na Ktk sherehe mbali mbali zitakazofanyika hapa Dar Inshaallah!!


"Lakini kubwa kwa wale wasiokuwa invited kuangalia Tafrija kubwa itayorushwa live na Channel ya sinemazetu ya Azamtv, tokea katika hoteli ya Serena siku ya Jumamosi!!


"Naomba Dua zenu Ndoa yetu iwe ya kheri na tuishi kwa amani na furaha mm na Laaziiz wangu kipenzi Naheeda” ameandika Manara.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

  1. Haji, Inshallah M/Mungu ajaalie ndoa ya Kheri na Masikilizano.

    Mungu akujalieni kizazi Chema, Tuko pamoja kesho inshallah.

    ReplyDelete