Haji Manara Atoa MPYA "Hivi Nikiondoka SIMBA Namuachia Nani Ukubwa wa Jina Langu Unaniponza?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Idaya ya Habari na Mawasilino Simba SC, @hajismanara amewajibu baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wamekua wakimtabiria mabaya kuhusu kazi zake ndani ya klabu hiyo.


#Manara ametuma majibu hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kufuatia madai yaliyotolewa na baadhi ya wadau hao wakisema amesimamishwa kazi, huku akitakiwa kutozungumza lolote kuhusu Simba SC.


#Manara ameeleza kuwa, bado yupo Simba SC, na ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida, huku akiwatuliza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


“Please Please Please (Tafadhali) Wanasimba mimi Haji wenu bado nipo nanyi na nitaendelea kuwa msemaji wenu hadi pale riziki yangu itakapokwisha, (Hatatokea mmoja wetu kubaki milele iwe kwa kifo au vinginevyo).


“Waambieni wenye kuandika tetesi za kuondoka kwangu, mimi mtu dhaifu lakini ni mjuzi mno katika mambo ya mawasiliano ya umma na nina uzoefu mkubwa katika eneo hili na nishakuwa sugu na changamoto za kazi.”


“Halafu waulizeni Simba namuachia nani ? Alihoji @hajismanara


#Manara amedai kuwa, huenda ukubwa na umaarufu wa jina lake unamponza hadi kufikai hatua ya kuzushiwa mambo kama hayo, lakini anahisi huenda hatua ya kuzushiwa majanga inatokana na kazi yake kuwavutia wengi ndani na nje ya nchi.


“Huu ukubwa wa jina langu unaniponza, umaarufu wangu unawaumiza wengine. “Sikuwahi kutaka kuwa hivi, lakini kazi yangu naamini imewavutia wengi na Mungu akaamua kunipandisha.”


Ikumbukwe, #Manara aliwahi kutoa ufafanuzi kwa nini amekua kimya kwa majuma kadhaa, akisema uongozi wa Simba SC ulimpa mapumziko (Likizo) baada ya kufunga ndoa na mke wake Naheeda Abdallah, Desemba 10 mwaka huu 2020.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad