Harmo Aundiwa Hujuma Nzito

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rajab Abdul ‘Harmonize’ hivi karibuni ameundiwa hujuma nzito baada ya kudaiwa kuacha kufanya kazi na mmoja wa meneja wake anayefahamika kwa jina la ‘Jembe ni Jembe’.


Akizungumza na RISASI JUMAMOSI, meneja mwingine wa msanii huyo, Beauty Mmari alisema tetesi hizo hazina ukweli wowote kwa sababu wawili hao bado wapo pamoja na wanaendelea kupiga kazi kama kawaida.


“Hizo habari hazina ukweli wowote ule, Jembe na Harmo hawajagombana, bado wapo pamoja na wanaendelea kupiga kazi kama kawaida, pia Jembe anatoa sapoti ya kutosha kwa Harmo kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Beauty.


Hata hivyo, baada ya kuzungumza na meneja huyo RISASI lilifanya jitihada za kumtafuta Jembe mwenyewe ambapo alipopigiwa simu mara kadhaa alikata na kuomba atumiwe ujumbe mfupi wa maneno hata alipotumiwa hakujibu chochote.


ISHU NZIMA ILIVYOKUWA


Awali zilianza kusambaa tetesi mitandoani kuwa Harmo haelewani na Jembe ni Jembe ambaye ni miongoni mwa mameneja wake ambao kimsingi ndio humsaidia kumsogeza mbele kimuziki.

“Jamani eeh, kumekucha inasemekana kwamba Harmo kagombana na Jembe ndio maana siku hizi kabuma, hata shoo zake ana-promote mwenyewe huku Jembe yeye yupo bize na maisha yake,” aliandika shabiki mmoja katika mtandao wa Instagram.


Madai hayo yalizidi kushadadiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa, hata kwenye tuwa ya Ushamba ambayo Harmo ameanza kuifanya pande za Mtwara, meneja huyo hakuonekana pande hizo.

Hata hivyo, baadhi ya wachangiaji katika taarifa hiyo, walidai ni hujuma zinazolenga kimshusha kimuziki jambo ambalo si zuri kwa afya ya sanaa hiyo nchini.

STORI: MEMORISE RICHARD

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments