google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Haya Ndiyo Majimbo Aliyoyatarajia Prof. Ibrahim Lipumba | UDAKU SPECIAL

Haya Ndiyo Majimbo Aliyoyatarajia Prof. Ibrahim Lipumba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUf), Prof. Ibrahim Lipumba amezindua  rasmi kongamano  lenye lengo la kutetea maslahi na haki za wananchi nakusema kuwa uchaguzi wa mwaka huu alitegemea kuchukua viti 15 kwa upande wa ubunge.


Akizungumza katika uzinduzi wa kongamano hilo la Kudai katiba mpya, Mwenyekiti wa CUF,  Prof. Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa mgeni rasmi amelishukuru jeshi la polisi nchini kwa kuwaacha kuendelea na kongamano lao huku akihimiza kuzingatiwa kwa demokrasia nchini .


"Mkoa wa Kilimanjaro wamekuwa wanatoa wabunge wa upinzani lakini mwaka huu majimbo yote yamechukuliwa na wote wameenda kuunga juhudi, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 mimi nilikuwa na uhakika tutapata walau viti 15 vya ubunge" amesema Prof. Lipumba


Aidha Prof.Lipumba amemuomba  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuanza kusikiliza hoja za watanzania kuhusiana na suala la katiba mpya.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad