Hoteli ya Kitalii ya Ngurdoto Yageuzwa Hosteli
HOTELI ya kitalii ya Ngurdoto Mountain Lodge yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Arumeru mkoani Arusha, imegeuzwa hosteli ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) baada ya kufungwa kwa siku kadhaa kutokana na ukosefu wa wateja, baada watalii kutoka nje kupungua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19 duniani.

 

 

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Eliamani Sedoyeka, amethibitisha chuo chake kuingia mkataba na Kampuni ya Landmark inayoisimamia hoteli hiyo na kwamba wamepata nafasi ya kutosha malazi ya wanafunzi 1,000, huku kila mmoja akitakiwa kulipa sh. 400,000 kwa mwaka.

 

 

Ameongeza kwamba wanaendelea na mazungumzo ya kutumia kumbi za mikutano hotelini hapo kama madarasa huku pia wakifikiria kuongeza vitanda vitakavyowatosha wanafunzi 2,000.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments