Huu ndio uteuzi alioufanya Rais Magufuli leoRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzabnia, Dkt. John Magufuli, amemteua Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi, Jaji wa Mahakama ya Rufani kuwa Kamishna wa Maadili, akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Harold Nsekela aliyefariki dunia.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Taarifa hiyo imetolewa leo  Desemba 23, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambapo ameeleza kuwa uteuzi huo umeanza hii leo na ataapishwa kesho Desemba 24, 2020, Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa umma, Harold Nsekela, alifariki dunia Jumapili ya Desemba 06, 2020, baada ya kuugua kwa muda mfupi.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments