Huyu Nd’o Naibu Waziri Aliyeshindwa Kuapa Mbele ya JPM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA





RAIS John Magufuli amesema atamteua naibu waziri mwingine wa madini baada ya aliyemteua Desemba 5, 2020, Francis Ndulane, kushikwa kigugumizi wakati akila kiapo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatano Desemba 9, 2020.


Ndulane ambaye ni mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) mwenye elimu ya shahada ya uzamili ameshindwa kusoma kiapo mbele ya Magufuli, akikosea mara kadhaa kila alipopewa nafasi ya kurudia kusoma na ndipo katibu mkuu kiongozi, John Kijaz,i kumtaka aende kuketi kwanza.


Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge, Ndulane ana elimu ya shahada ya uzamili katika uhasibu na fedha ambayo ameisomea katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 na 2015. Pia, ana stashahada ya juu ya uhasibu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM).


Ndulane alisoma shule ya msingi Uwanjani (mwaka 1980 – 1986), baadaye akaenda sekondari ya Tambaza (mwaka 1987 – 1990) na baada ya kuhitimu kidato cha nne, alikwenda Sekondari ya Pugu (mwaka 1991 – 1993).

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad