Ibrah Atangaza Balaa la Kufungia Mwaka
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, chini ya Lebo ya Konde Gang Music Worldwide, Ibrahim Abdul ‘Ibrah’ ametangaza balaa la kufunga mwaka kwa kuachia ngoma tatu kwa mpigo ambazo amezipa jina la Karata Tatu.

 

Akizungumza na Amani juu ya ujio ya ngoma zake hizo Ibrah amesema kuwa, kwa upande wake anafanya hivyo ili kuweza kuwapatia mashabiki wake kitu ambacho wanakipenda.

 

“Karata Tatu imesheheni nyimbo kama Mapenzi, Upande na Nimpende. Nimeamua kufanya hivyo ili kuweza kuwafurahisha mashabiki wangu,” alisema Ibrah.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments