Jeshi la Ethiopia 'lawaua washukiwa 40' Benishangul-Gumuz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA






Jeshi la Ethiopia limewaua zaidi ya watu 40 wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya zaidi ya watu 100 ikiwemo watoto katika eneo la Benishangul-Gumuz , vyombo vya habari vimesema.


Maafisa watano wa serikali ya sasa na wenzao wa zamani pia walikamatwa kufuatia tatizo hilo la kiusalama , ripoti zimeongeza.



Washukiwa hao walichoma nyumba za wanavijiji waliokuwa wamelala kuwapiga risasi na kuwachoma visu wakati wa shambulio hilo la siku ya Jumatano.



Shambulio hilo linajiri siku moja baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kuzuru eneo hilo.



Haijulikani washambuliaji ni akina nani lakini walionekana kulenga jamii za makabila madogo yaliowasili na kuishi katika eneo hilo , kulingana na Amnesty International.



Ethiopia imeshuhudia ongezeko la ghasia za kisiasa, kikabila na kidini katika miaka ya hivi karibuni.



Ilikuwa na idadi kubwa ya watu waliowacha bila makao barani Afrika 2018 takriban watu milioni 1.8.



Mizozo kwa kiwango kikubwa imechochewa na makundi yanayopigania ardhi zaidi na uwezo wakijaribu kuwafukuza watu wanaodaiw kutoka sehemu nyengine.



Mr Abiy alielezea mauaji hayo kama ya kusitisha na kusema kwamba serikali yake imetuma wanajeshi katika eneo hilo ili kutafuta suluhu ya mzozo huo.



Vyombo vya habari vya serikali havikutoa utambuzi wa watu hao 42 katika operesheni hiyo ya kuwasaka washambuliaji.



Vilisema kwamba silaha ikiwemo mishale ilikamatwa ilisema ripoti ripoti hiyo.



Naibu waziri wa serikali ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa vilisema vyombo vya habari vya serikali.



Miongoni mwa watu hao watano waliodaiwa kuhusika na mzozo huo huku wengine walikamatwa kwasababu hawakufanya jukumu lao , ripoti hizo zilisema.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad