JPM Amtumbua Mkurugenzi Aliyenunua Gari la Mil 400
RAIS John Magufuli amemuagiza Waziri wa Ofisi ya Rais -Tamisemi, Suleiman Jaffo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Aporinary, kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Serikali ambazo ni Sh Milioni 400 zilizolenga kuhudumia wananchi lakini akanunua gari la kutembelea.

 

Ametoa agizo hilo leo Jumatano, Desemba 9, 2020 wakati akiwaapisha mawaziri na naibu mawaziri Ikulu Chamwino Dodoma.

 

“TAMISEMI kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo Suleiman Waziri wa TAMISEMI umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha.

 

“Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndiyo kazi yako ya kwanza ukaanze nayo.

 

“Juzi tumekamata magari saba yaliyobeba chuma chakavu, havikuwa vyuma chakavu, tunajenga reli ya kisasa kwa zaidi ya Trilioni 7 halafu kuna wengine wanaiba, na katika wahusika yumo OCD wa Mlandizi na Mkuu wa Kituo na niliagiza waondolewe nina imani IGP umeshawaondoa.

 

“Hili lilitakiwa liwe limeshashughulikiwa, ndiyo maana nimempeleka pale Ummy Mwalimu akatumie sheria yake vizuri na Mwita Waitara akatumie amri ya Kikurya. Kila Mtanzania anapaswa kufahamu wajibu wake ambao ni uzalendo, utaifa na kulinda maslahi ya taifa, siku moja tukikubali kuchezewa tutajuta maisha yetu yote,” amesema Magufuli.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments