JPM Kumtumbua Naibu Waziri Aliyeshindwa Kuapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli, amesema atafanya uteuzi mpya wa Naibu Waziri wa Madini baada ya aliyemteua, Francis Ndulane kushindwa kuapa.

 

Amesema hayo leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, muda mchache baada ya kumaliza kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma. Rais Magufuli amesema hayo, wakati akichambua wizara moja baada ya nyingine pamoja na mawaziri na naibu wao.

 

“Tumeangalia nafasi ya mikoa, ndiyo maana tumekuja na ninyi na tuna akiba nyingi sana kwa hiyo tukibandua tu, tunabandika kingine. Ninawaomba mkajitume sana na kuwatumikia wananchi. Tume ‘balance’ wazee na vijana, kuna mzee George Mkuchika amekuwamo wakati wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Hata mimi kwenye baraza nataka wazee na hata ushauri wao na lazima tuzitunze hazina zetu.

 

 

“Ninawafahamu wote niliowateua, mpaka wewe uliyeshindwa kuapa. Nafikiri nitamtafuta mwingine anayejua kuapa vizuri. Waziri Mkuu ananiangalia kwasababu Lindi wametoka yeye na huyu aliyeshinda kuapa, sasa tutamteua mwingine na wewe tutacheki ‘Degree’ yako vizuri, Tunakupongeza utaendelea kuwa mbunge,” amesema Rais Magufuli.

 

“Kuna Mbunge tulimfukuza kwenye vyeti feki leo ameenda amefamba na kawa Mbunge, ila kwa kuwa ‘qualification’ ya Ubunge ni kusoma na kuandika, na wewe uliyeshindwa kuapa tutachunguza vyeti vyako na tutamteua mwingine, mambo ya kuchomekewa yapo.

 

Rais Magufuli amesema, lazima kuwe na naibu waziri anayeweza kusoma vizuri nyaraka mbalimbali ili asije kusaini nyaraka za muhimu bila kusoma kwa umakini. Wakati wa kiapo, Kumba alikuwa akikosea kusoma kiapo kwa kurudia rudia hali iliyomfanya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kumpa maelekezo.

 

Hata hivyo, Ndulane ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM) hakumaliza kiapo chake kwa Balozi Sefue kumwomba aende akampumzike kwanza ili kupisha wengine kuendelea kuapishwa.

 

Kwa mujibu wa wasifu wa Ndulane uliowekwa katika tovuti ya Bunge la Tanzania, inamwonyesha ana shahada ya uzamili ya uhasibu na fedha aliyoipata Chuo Kikuu cha Mzumbe kati ya mwaka 2013 hadi 2015.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. JPM Baba, Lindi Wabaya..!! Walimfanyizia Bi Husna Saidi Mwambiko wa UVCCM .

    Ni mdada binti mtanashati lakini aliingia kigugumizi kisicho na mwanzo... Mpe fursa mteule wako na umsikilize.

    ReplyDelete

Top Post Ad