Kahama: Babu wa Miaka 75 Akamatwa na Silaha za Kivita

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




POLISI  mkoa wa Shinyanga linamshikilia Masanja Maziku Bugolole (75) Mkazi wa Kijiji cha Gula Wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma ya kumiliki silaha nne aina ya Shotgun, mitutu sita ya Shotgun na Risasi 36 kinyume cha sheria.



Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani Kahama, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Debora Magiligimba, alisema kuwa Masanja alikamatwa Desemba 17 mwaka huu majira ya usiku nyumbani kwake kufuatia msako maalumu unaoendeshwa na jeshi hilo kwa lengo la kuwakamata wahalifu mbalimbali.



Alisema kuwa silaha zilizokamatwa zimebainika kufutika namba zake za uhakiki na zingine zina namba lakini hazijasajiliwa kama sheria za umiliki wa silaha zinavyoelekeza sambamba na kutokuwa na kibali cha kumiliki risasi 36 ambazo alikamatwa nazo.



“Silaha moja imebainika kuwa na uhakiki wa namba TZCAR 34951 lakini usajili wake umefutika, silaha tatu hazina namba za uhakiki lakini zina namba za usajili ambazo ni silaha namba D 172321,14999 na 24162,”alisema Magiligimba.



Aliongza kuwa baada ya upelelezi kukamilika Masanja atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.



Sambamba na hilo Magiligimba alifafanua kuwa katika msako huo pia jeshi hilo liliokota silaha mmoja aina ya Gobole katika kijiji cha Mpera wilayani humo ikiwa imetelekezwa kichakani na kuwataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kutoa taarifa za watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad