Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kampuni Yalipwa Mamilioni Kulinda Biden Akiapishwa

 


RAIS Mteule wa Marekani, Joe Biden anatarajiwa kulindwa na kampuni maalum ya ulinzi ambayo italipwa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwenye tukio la kuapishwa kwake, Januari 20, 2021.

 

Nyaraka ambazo Mtandao wa TMZ umesema unazo, zimeonesha kuwa Shirika la Ujasusi la Marekani (Secret Service) limeipa tenda ya ulinzi Kampuni ya Showcall Security Services kuwasaidia ulinzi kwenye tukio hilo la kihistoria.

 

Nyaraka hizo zimeonesha, kampuni hiyo inatarajia kulipwa kiasi kisichopungua Dola Milioni 7.5 ( zaidi ya Shilingi Bilioni 18) kama sehemu ya mkataba huo wa muda mfupi ambapo watahakikisha siku hiyo kunakuwa na ulinzi wa kutosha kwenye maeneo mbalimbali.


 

Biden wa Chama cha Democratic, alichuana na Donald Trump wa Chama cha Republican katika Uchaguzi Mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 3, 2020.

 


 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments