Kaseke Aahidi Mabao 15 Yanga
BAADA ya kufanikiwa kufikisha mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara, kiungo wa Yanga, Deus Kaseke amesema kuwa ataweka jitihada zaidi kila anapopata nafasi ili afunge zaidi na ikiwezekana mwisho wa msimu afikishe mabao 15.

 

Kaseka aliongeza kuwa, kadiri anavyozidi kufunga uwezo wake wa kujiamini unazidi kuongezeka na hiyo inamsaidia yeye katika kuyakimbilia malengo yake ya kutaka kufikisha mabao 15 msimu huu.

 

Kaseke amefunga mabao hayo matatu katika michezo minne aliyocheza hivi karibuni, akifunga bao la ushindi mbele ya Azam FC mchezo ukimalizika kwa Yanga kushinda 1-0 pale Azam Complex, Chamazi, kisha akawapa tena ushindi mbele ya JKT Tanzania, Yanga wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 pale kwa Mkapa na kisha akifunga moja wakati Yanga akishinda 5-0 dhidi ya Mwadui.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaseke alisema: “Kwanza nashukuru Mungu kwa kuwa naendelea kupewa nafasi na mwalimu, siyo jambo dogo kucheza mara kwa mara kwenye timu hii ya sasa. Kuhusu kufunga ni ushirikiano kwanza na wenzangu pamoja na jitihada binafsi.

 

“Kufunga mara kwa mara kunaniongezea kujiamini zaidi, nafikiri kama nitakuwa salama hadi mwisho wa msimu, Wanayanga watarajie mabao 15 kutoka kwangu, tuombe Mungu tu.’

STORI NA ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments