Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Kauli ya Maalim Seif baada ya Kuapishwa

 


Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka Wazanzibar waliondani na nje ya nchi wakubali kuunga mkono maridhiano kwa kuzika historia na majeraha yaliyopita ili kuijenga Zanzibar iliyobora.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 8, 2020, wakati akizungumza mara baada ya kula kiapo cha nafasi hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi, Ikulu ya Zanzibar.


"Nitoe wito kwa Wazanzibar wote waliondani na nje ya nchi, wakubali kunyoosha na kupokea mkono wa maridhiano, tumeze machungu yanayotokana na uchaguzi, historia yetu imejaa majeraha ya kila aina ni wakati wa kuzika historia hiyo na kushikamana na kuijenga Zanzibar yetu", amesema Maalim Seif.


Aidha akizungumzia sababu iliyopelekea wao kuingia katika maridhiano na kukubali kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif amesema kuwa, "Moja ya sababu zilizotufanya tufikie uamuzi huo ni imani yetu kwako, maneno yako, vitendo na ishara zako ambazo zimetushawishi kuwa unayo nia njema na dhamira safi ya kututoa tulipokwama na kuibadilisha Zanzibar yetu katika nyanja zote na wewe ni mtu tunayeweza kufanya kazi na kusikilizana". 

  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

1 Comments

  1. Hongera Seif. hii inaitwa Busara.

    Chapa Kazi kwa moyo mmoja kumsaidia Rais Mwinyi, kuleta Zanzibar Mpya. zanzibar kwanza. Siasa Baadae.

    Shikamaneni katika kuijenga nchi. Dira ya Dkt Mwinyi iko wazi na ina mwelekeo like never B4.Hilo mulielewe.

    ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)