Kigwangalla Amemmisi Shangazi Amfungukia Haya TWITTER, Shangazi Naye Amjibu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, pamoja na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa mtandao wa Twitter na huwa wanamijadala mbalimbali.

Baada ya muda mrefu Kigwangalla kuwa kimya kidogo kwenye mtandao huo, hivi karibuni alirejea na wafuasi wake wakampokea kwa furaha huku mmoja wa wafuasi hao akimkumbusha kuwa anaporejea ni lazima ajue Fatma Karume yupo anamsubiri.


Kigwangalla alimjibu kwa kushangaa kama Fatma maarufu Shangazi bado yupo na akahoji kama ataendelea kumsakama kama alivyokuwa anafanya wakati akiwa Waziri.


Hivi Shangazi bado yupo? Anasemaje? Sijui ataendelea kunisakama ama atanihurumia maana sasa sina cheo tena! — Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) December 27, 2020


Lakini kwa upande wa pili Fatma Karume amejitokeza na kumjibu Kigwangalla kuwa yeye bado yupo na ataendelea kama ilivyokuwa zamani.


@HKigwangalla kumbe hukuelewa kuwa uwaziri unakuja na Marafiki? Pole ndugu yangu. Lakini elewa I never abandon watani wangu. Utani upo pale pale hata kama si Waziri tena. — fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) December 27, 2020

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad