Kikosi cha simba kuondoka leo kuwafuata FC Platinum LEO Desemba 18 kikosi cha Simba kinatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Wachezaji watatu wanatarajiwa kubaki ndani ya ardhi ya Bongo wakiendelea kufanya program ambazo wataachiwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck. 


Wachezaji hao ni pamoja na Charles Ilanfya ambaye ni mshambuliaji namba nne wa Simba,Larry Bwalya ambaye ana matatizo ya kifamilia na Thadde Lwagga ingizo jipya ndani ya kikosi.


Simba itacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.


Ikiwa itashinda kwenye mchezo wa kwanza na kuweza kulinda ushindi wake kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa Bongo, Simba inaweza kutinga hatua ya makundi

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments