Kilichomkosesha Mwana Fa kwenye Album ya Darassa

 


Mbunge wa Jimbo la Muheza na msanii wa HipHop Mwana Fa, amesema kutokana na ratiba na majukumu yake kuwa mengi nusu ya mwaka 2020 ndiyo imemfanya kukosa Album ya Darassa 'Slave Become A King'

 

"Nilitaka sana kuwemo kwenye hii album ratiba tu hazikunikubalia, nusu hii ya pili ya mwaka 2020 ratiba zangu zilibebwa na majukumu mengine na nimekosa kabisa muda wa kurekodi chochote, nimesikitika lakini silalamiki kwa sababu najua 'my brother' Darassa ni mtu 'serious' sana na hawezi kuniangusha, ni imani yangu tupo tayari" ameeleza Mwana Fa 


Darassa amezindua Album yake ya 'Slave Become A King' ikiwa ni ya kwanza tangu alivyoanza muziki ambayo ina jumla ya nyimbo 21 huku akiwashirikisha wasanii kama Dogo Janja, Billnass, Alikiba, Juma Nature, Rich Mavoko, Barakah The Prince, Ben Pol, Sho Madjozi, Maua Sama, Kassim Mganga, Eddy Kenzo na Wini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments