Kim Kardashian Kwenye Majonzi Makubwa...Aliyenyongwa na TRUMP Aliyekuwa Mfungwa Mmoja Wapo Aliyekuwa Anamtetea


Kim Kardashian amempoteza miongoni mwa watu ambao alikuwa akiwatetea kwenye kesi zao mahakamani. Brandon Bernard amenyongwa hadi kufa Jana mjini Texas Marekani.

Haikuwa siku nzuri kwa Kim Kardashian ambaye kwa muda mrefu alipambana na kesi hiyo ya mauaji akiiomba mahakama kumpunguzia adhabu Brandon kwa kuwa ana familia.

Brandon Bernard alitekeleza mauaji ya watu wawili (Todd na Stacie Bagley) mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 18, baada ya wenzake kuwaua kwa risasi, Brandon aliingiza miili kwenye gari na kuiwasha moto.

Kim Kardashian alikutana na upingamizi mkali toka kwa ndugu wa marehemu. Lana Ladd alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha Brandon anauawa pia, huku akimshukia Kim K kwa kumwambia hana uchungu kwa sababu waliouawa sio ndugu zake


"Kim Kardashian inabidi aache kujaribu kumsaidia muuaji Brandon Bernard kwenye adhabu ya kunyongwa kwa sababu hapati maumivu kwa familia aliyoiharibu [Brandon]" alisema Lana. Brandon alinyongwa jana mishale ya Saa 9:27 Usiku kwa saa za Marekani.

That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments