Kimenuka..Mfanyakazi wa TANESCO apandishwa kizimbani kwa kuhujumu mradi SGR

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mfanyakazi wa TANESCO mkazi wa Kibaha kwa Mathias Mkoani Pwani amefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam ikiwemo kosa la uhujumu kwakuingilia  miundombinu ya umeme ya reli ya kisasa ya SGR nakuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya shilingi milioni sitini na mbili.


Kesi hiyo ya uhujumu  namba 95 ya mwaka 2020 imesomwa na wakili wa Serikali Mkuu Martenus Marando   mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Kisutu  Kassian Matembele ambaye amedai kuwa mshitakiwa Godfrey Maleko ametenda kosa hilo Mei 15,2018 maeneo ya TANESCO  Majani ya Chai jijini Dar es Salam.



Wakili Marando amedai mshitakiwa Maleko aliiba nyaya hizo zenye urefu wa mita  403 ambazo zimetengwa kwa ajili  mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR nakuisababishia Serikali kiasi kilichotajwa.


Baada ya kusomewa mashashitaka yanayomkabili mshitakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.


Hata hivyo Wakili Marando amedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo akaomba mahakama kupanga  tarehe nyingine  kwa ajili ya kutajwa kwa  shauri hilo.


Baada ya kusikiliza hoja za upande wa Mashtaka Hakimu Matembele amehirisha kesi hiyo  hadi Decemba 17 mwaka huu.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad