google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Kizimbani kwa kusambaza maudhui bila kibali | UDAKU SPECIAL

Kizimbani kwa kusambaza maudhui bila kibali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



MFANYABIASHARA anayeishi Kinondoni Bwawani jijini Dar es Salaam,  Benedict Kimbusu, amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka kusambaza maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Adolph Ulaya, mbele ya Hakimu Mfawidhi Yusto Ruboroga imedai kuwa mshtakiwa ametenda hilo, kati ya Februari 27, 2014 na Desemba 7 mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam. 

Imedaiwa, siku hiuo, mshtakiwa alisambaza maudhui kupitia Chanel ya YouTube iitwayo Pioh the 9os Lyrics bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka ya mawasiliano TCRA.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana ya kufanikiwa kutimiza masharti ambayo yaliyomtaka kuwa na wadhamini watakaosaini bondi Bondi ya sh. Milioni tatu. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa Desemba 30, mwaka huu.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad