Klopp Awajibu Wanaosema Salah Hana Furaha Liverpool


Kama ulidhani Mohammed Salah kwasasa hana furaha Liverpool, basi unajidanganya na haiko hivyo, Kocha wa Majogoo hao wa Jiji la Liverpool, Jurgen klopp amezipiga chini taarifa hizo alizoziita ni uzushi.


“Salah ana furaha, hilo ndilo jambo muhimu kwasasa, hatukupiga picha tukiwa mazoezini, ila umeona jinsi alivyokuwa akifurahi” amesema Klopp.


Salah aliyaambia magazeti ya Hispania kuwa alichukizwa kufuatia kutokuwa nahodha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Midtjyland na badala yake kitambaa cha unahodha alipewa Alex Anord.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments