Kocha Simba Afunguka Sababu za Kumpanga Kagere

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amefunguka sababu ya kubadili kikosi chake cha kwanza kwa kuwatumia wachezaji wengi ambao hawapati nafasi kikosini hapo katika mchezo wa juzi dhidi ya Polisi Tanzania.


Mbelgiji huyo aliwatumia Meddie Kagere, Gadiel Michael, Bernard Morrison, Francis Kahata na Ibrahim Ame ‘Varane’ katika kikosi cha kwanza cha mchezo huo.

Sven alisema mwezi huu wa Desemba kila baada ya siku tatu wana mechi hali inayowasababishia wachezaji kuchoka, ndiyo maana ameamua kufanya mzunguko wa mara kwa mara.


“Hiyo itawasadia wachezaji wangu kupunguza uchovu na majeraha yatakayotokana na kutumika muda mrefu.

“Kwenye mchezo wetu huo (dhidi ya Polisi) tulitengeneza nafasi nyingi na tulimiliki sehemu kubwa ya mchezo lakini kikubwa nimeridhika na kiwango tulichoonyesha,”


Sven ambaye timu yake ilishinda kwa mabao 2-0.

Kagere awatuliza mashabikiAidha, Kagere amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna tofauti yoyote kati yake na Sven.


“Sina tatizo na kocha na wala kocha hana tatizo na mimi kwenye timu yetu hakuna tatizo lolote, hivyo niwaombe mashabiki wetu wawe watulivu malengo yetu kama timu ni kuhakikisha tunanya vizuri kwenye kila mchezo tutakaocheza.


Stori: Wilbert Molandi na Hussein Msoleka, Dar

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments