Kocha wa Serengeti boys awapongeza Navy Kenzo kwa academy yao ya mpira, awataja Diamond na Samatta katika hiliKocha mkuu wa timu ya taifa ya Serengeti Boys leo amewapongeza wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao wanaunda kundi la Navy Kenzo kwa kuanzisha Academy ya mpira wa miguu ambayo inafanya vizuri kwa sasa.

Akiongea na bongo5 amesema kuwa Academy hiyo ya Navy Kenzo Academy imetoa wachezaji watatu wanaounda timu hiyo ya taifa ya chini ya miaka 17 ambayo inajiandaa kwenda kushiriki mashindano ya AFCON nchini Rwanda.

Mbali na kuwapongeza Navy Kenzo pia amemuomba Diamond asikate tamaa na kuacha kuandaa Academy yake ambayo alitangaza ataianzisha muda sio mrefu.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments