Kumbe Lil Wayne hakuuza tu Master Recording zake kwa Universal Music Group, Unaambiwa Kauza Mpaka za Drake na Nick Minaj


Kumbe Lil Wayne hakuuza tu Master Recording zake kwa Universal Music Group, taarifa zinaeleza kwamba ameuza mpaka Master Recording za Young Money.


Wiki iliyopita zilitoka taarifa hizo ambapo Wayne alidaiwa kukunja kibindoni kitita cha ($100M) takribani Bilioni 231 za Kitanzania kwa kuuza nakala halisi za kazi zake kwa Universal Music Group.


Kwa mujibu wa TMZ anbao wana wingi wa taarifa hii, wameripoti kwamba Lil Wayne ameuza hadi Master Recording za Young Money zikiwemo za Drake na Nicki Minaj kwa dau hilo hilo tajwa hapo juu.


Hii imehusisha album za Drake ikiwemo Take Care, Nothing Was the Same na Views hadi Scorpion ya 2018, album yake ya mwisho chini Label hiyo. Kazi zingine zilizouzwa ni za Nicki Minaj, album zake zikiwemo: Pink Friday, The Prinkprint na Queen.


Una maoni gani kuhusu uamuzi huu wa Lil Wayne? Tuachie comment yako.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments