Maafisa 2 waliompiga mwanamuziki wa Kiafrika wakamatwa

 


Maafisa wawili wa polisi waliompiga mwanamuziki wa Kiafrika Michel Zecler nchini Ufaransa wamekamatwa.

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa, jaji wa uchunguzi alielekeza kesi hiyo kwa mwendesha mashtaka inayowakabili maafisa 4 wa polisi waliofikishwa mahakamani.


Maafisa 3 kati ya 4 walioshutumiwa, walikabiliwa na mashtaka ya "matumizi ya silaha kwa makusudi kueneza vurugu za kibaguzi na ubandia wa nyaraka rasmi."


Afisa wa nne wa polisi ambaye baadaye aliingilia kati tukio hilo na kutumia bomu la machozi, alishutumiwa kwa ‘’makabiliano ya kimabavu’’


Jaji wa uchunguzi aliamua kuwakamata maafisa 2 wa polisi na kuwaachilia wengine 2 kwa sharti la udhibiti wa kimahakama.


Mnamo Novemba 21, siku ya Jumamosi, mtayarishaji muziki Zecler alikumbana na shinikizo za polisi kwenye studio iliyoko eneo la 17 mjini Paris, ambapo maafisa 3 kati yao walikuwa wamevalia sare za kazi.  Majirani waliosikia kelele za Zecler za kuomba msaada baada ya kupigwa kwa dakika 20, waliingia kwa mlango wa nyuma ili kumsaidia.


Baada ya kuwaona majirani, maafisa wa polisi walimwacha Zecler na kuondoka studio ili kuita kikosi cha usalama. Afisa wa polisi wa kikosi cha usalama aliyewasili kwenye eneo la tukio, alirusha bomu la machozi ndani na kumtoa nje Zecler.


Baada ya picha za kamera za usalama  zilizorekodi tukio la Zecler aliyewekwa chini ya ulinzi na polisi kwa masaa 48, kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris ilimwachilia huru Zecler. Baadaye  maafisa 4 wa polisi walisimamishwa kazi kwa kutumia nguvu kwenye makabiliano.

 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments