Madaktari Njia Panda Mama ‘Kujifungua’ Kuku

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



WAKATI Ofisi ya Mkemia mkuu mkoa wa Mwanza ikisubiriwa kutoa majibu ya uchunguzi kuhusu mwanamke ‘aliyejifungua’ kuku mkoani Kigoma, madaktari wamebaki njia panda na kusisitiza kuwa tukio la binadamu kujifungua ndege haliwezi kutokea.

 

Kauli hiyo ya madaktari imekuja siku chache baada ya mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Kalelwa wilayani Uvinza mkoani Kigoma kuwashangaza madaktari na wahudumu wa afya katika kituo cha afya Uvinza baada ya ‘kujifungua’ kuku badala ya mtoto.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk Simon Chacha alithitisha kutoka kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwanamke huyo alifika kituoni hapo kupatiwa matibabu akiwa na maumivu makali ya tumbo, “baada ya vipimo na uchunguzi waliona miguu ya kuku katika mfuko wa kizazi wa mwanamke huyo.”

 

Alisema utaratibu ulifanyika na kufanikisha kutoa kifaranga ndani ya mfuko wa kizazi wa mwanamke huyo.

 

MADAKTARI WANENA

Aidha, madaktari waliozungumza na UWAZI, akiwamo Dk. Godfrey Chale ambaye ni mtalaamu wa masuala ya akina mama na watoto, alisema ndege hana uhusiano wowote wa vinasaba na binadamu.

 

“Afadhali angejifungua viumbe wenye vinasaba na binadamu kama nyani au sokwe, lakini sio ndege,” alisema.

 

Hoja hiyo na Dk. Chale iliungwa mkono pia na Dk. Sadick Sizya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye aliongeza kuwa licha ya kwamba wataalam hao wa afya hawaamini katika masuala ya ushirikina, lakini kiujumla suala la binadamu kujifungua ndege haliwezi kutokea.

 

“Sijui nifafanue vipi, ila inawezekana kukawepo na udanganyifu wa aina yoyote, labda mama alikuja na ndege huyo akiwa amemficha kwenye nguo ya ndani au lah. Lakini ni jambo linalohitaji uchunguzi wa kina, haiwezekani mtu kujifungua kuku,” alisema.

 

TUKIO LILILOVYOTOKEA

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, ACP James Manyama alisema tukio hilo lilitokea Desemba 5, 2020 saa tatu usiku katika kituo cha afya Uvinza.

 

Alisema mwanamke huyo alifika katika kituo hicho akiongozana na mumewe kwa ajili ya kujifungua, walipofika alipitishwa moja kwa moja wodini na mhudumu wa afya wakati akimpatia huduma mwanamke huyo alibaini hali isiyo ya kawaida kutokana na uzoefu wake.

 

“Alipoona hali si nzuri alimuita daktari wa zamu aliyekuwepo kituoni hapo ili waweze kusaidiana kumzalisha mwanamke huyo. Aliposukuma mtoto kilitoka kiumbe tofauti na mtoto…, alikuwa kuku ambaye hakuwa na manyoya.”

 

“Tukio hilo ambalo si la kawaida katika jamii zetu linahusishwa na imani za kishirikina ingawa Serikali haina imani na mambo hayo. Polisi walichukua kiumbe hicho na kukipeleka maabara ya mkemia mkuu mkoani Mwanza kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Manyama.

Uwazi

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad