Magufuli aagiza waliotoka TMAAna kuhamia tume ya madini kupunguziwa mshahara

Rais John Magufuli ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kuhamishiwa Tume ya Madini kupunguziwa mishahara yao waliyotoka nayo huko.


Ameeleza hayo leo Ijumaa Desemba 11, 2020 baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya Ikulu jijini Dodoma.Amesema wafanyakazi hao wamekuwa wakipokea mishahara mikubwa kuliko hata wakurugenzi wao.“Mmehamishwa kule mmekuja na mishahara yenu, ile mishahara katibu mkuu kiongozi ipunguzwe kwa sababu wale walitakiwa wawe retrenched kwa sababu kazi waliyoifanya TMAA ilikuwa ya ovyo lakini hatutaki kuhukumu generally.”“Haiwezekani wewe ukapelekwa kwenye Tume ya Madini kutoka kule na mshahara wa Sh10 milioni ukamzidi hata mkurugenzi wako wakati hata sio mkurugenzi, ukamzidi hata executive chairman ambaye yuko hapo anapokea sijui Sh5 milioni, wewe una Sh10 milioni,” amehoji.Amesema anayetakiwa kuzidiwa mshahara ni yeye ambaye anapokea Sh9 milioni wakati mtu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) anapata Sh15 milioni.Amesisitiza kwamba lazima wafanye mabadiliko ya kanuni katika Tume ya Madini na kupunguza mishahara ya wafanyakazi hao. Amesema kama kuna mtu hataridhishwa na uamuzi huo aache kazi.“Kama wapo ambao hawataki kuteremshwa, waache kazi,” amesema Rais Magufuli wakati akitoa maagizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi, John Kijazi.


 


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments