Magufuli Agoma Kunyonga Wafungwa 256RAIS John  Magufuli, amewapunguzia adhabu wafungwa 256  waliohukumiwa kunyongwa na kuagiza wapewe kifungo cha maisha gerezani.  Wafungwa hao ni wale waliohukumiwa kunyongwa katika uongozi wa muhula wa kwanza wa Magufuli

 

Ametangaza uamuzi huo leo Jumatano tarehe 9 Desemba 2020, katika hafla ya uapisho wa mawaziri 21 na manaibu waziri 23, iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

 

“Leo ni siku ya Uhuru, najua katika kipindi cha miaka mitano mpaka leo natakiwa niwe nimenyonga watu 256  waliohukumiwa kunyongwa, sijanyonga hata mmoja, na wale 256 kwa mamlaka niliyopewa, nawapunguzia kifungo cha kunyongwa,  sasa wafungwe maisha,” ameagiza.

 

“Wwatanyongwa na wengine, sijui Jaji Mkuu (Prof. Ibrahim Juma), inawezekana huyo atakayekuja atawanyonga,” aliongeza akisema ameshindwa kuchukua hatua hiyo kwa kuwa hataki kuwa muuaji.

 

“Sababu hao waliohukumiwa kunyongwa waliua, mimi sheria iliniambia niue 256, nani mwenye dhambi zaidi huyo alioua mmoja au mimi nitakaoua 256?” amehoji na kuongeza:

 

“Nimeshindwa, ninaomba mnisamehe kwenye hilo, kwamba mimi nitakuwa muuaji, sababu wenzangu waliua wawili, mmoja au watatu walihukumiwa kunyongwa.”

 

Wakati huohuo, Magufuli, amewapunguzia adhabu na kuwaachia huru baadhi ya wafungwa kati ya wafungwa 3,316, waliopendekezwa kwake na Kamishna Jenerali wa Magereza.

 

“Wako wengine 3,316  wana makosa madogo ya wizi wa kuku, wengine walitumikia kifungo chao kwa muda mrefu.  Kwa mujibu wa mapendeko yaliyoletwa na Kamishna Jenerali wa Magereza, nimekubali kuwapunguzia adhabu zao na wengine kuachiwa kwa mujibu wa sheria,” amesema.

 

Pia ameagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kushughulikia suala hilo ili wahusika wakafungwe maisha ili wakashiriki katika kufanya kazi.
 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

1 Comments

 1. Asante Baba JPM.
  M/Mungu atakurehemu akhera. Kwa Maandiko yake anasema
  "Anae Warehemu watu hapa duniani, Allah atamremu Akhera"

  Inshallahh, Allah akujaze Imani na Amani na ampe Shiffa
  Mama na kumuinua kitandani.

  Inshallah Fatiha tutafanya Nunge na Gadaffi. Salat Isha leo

  ReplyDelete