Mama mzazi wa MC Pilipili afariki dunia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


Mama mzazi wa mshereheshaji Emmanuel Matebe maarufu kama MC Pilipili, Mariam Matebe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 20, 2020, kwa ajali ya gari wakati akielekea ukumbini kwenye harusi ya mtoto wake maeneo ya Afrikana Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram MC Pilipili ameandika maneno haya, “Ulale salama mama yangu mpenzi Mariam Matebe, umetufundisha upendo na umefariki ukijariibu kuonesha upendo lala salama mpenzi". Ujumbe ulioambatana na picha za mwisho walizopiga muda mfupi baada ya mdogo wake wa kiume Thomas Matebe kufunga ndoa jana mchana Desemba 19.


Kwa mujibu wa familia mwili wa marehemu Mama MC Pilipili  utasafirishwa leo jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu Jijini Dodoma kwa ajili ya taratibu za maziko.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad