Matukio aliyoyafanya Lissu baada ya kurejea nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



liyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lissu, Julai 27, 2020, alikanyaga ardhi ya Tanzania kwa mara ya kwanza tangu alipoondoka nchini baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani kwake Dodoma, wakati akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.



Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA na aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.


Lissu aliwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, siku ya Jumatatu mchana akitokea Brussels, Ubelgiji, alikokuwa akifanyiwa matibabu, baada ya kushambuliwa mwaka 2017.


Maelfu ya wananchi wengi wakiwa wamevalia nguo zenye rangi ya chama chake na wengine wakipeperusha bendera ya chama hicho walijitokeza katika uwanja huo kumlaki, wakiongozwa na viongozi wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe pamoja na John Mnyika.


Katika hotuba zake mara baada ya kuwasili nchini, Lissu alitoa pole kwa Watanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa, ambaye alifariki dunia usiku wa kuamkia Julai 24, 2020.


Mbali na pole hizo Lissu pia alielezea mateso aliyoyapata mara baada ya shambulizi lile, huku akidai kuwa alitamani kuibusu kwa mara ya kwanza ardhi ya nchi yake lakini alishindwa kwa kuwa goti lake moja hawezi kulikunja kutoka na athari ya risasi alizoshambuliwa nazo, pia aliwashukuru Watanzania wote na wasio Watanzania waliojitolea kumuombea na kumpatia damu wakati alipokuwa hajiwezi.


Mbali na tukio la Lissu kuwasili nchini, pia alishiriki katika kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020, akipeperusha bendera ya kiti cha urais kupitia chama hicho, ambapo katika kampeni zake aliahidi mambo kedekede na alibahatika kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi na kufanya kampeni zake.


Baada ya mchakato mzima wa zoezi la uchaguzi mkuu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilimtangaza mshindi wa kiti cha urais kuwa ni Dkt. John Pombe Magufuli, wa CCM aliyepata kura milioni 12.5 sawa na asilimia 84, huku Lissu yeye akipata kura milioni 1.9.


Mara baada ya mchakato wa uchaguzi kukamilika, mshindi kutangazwa na Rais Dkt. Magufuli, kula kiapo cha kuendelea kuiongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya pili, mnamo Novemba 10, 2020, Lissu aliondoka nchini kurejea nchini Ubelgiji, huku akidai kuwa haondoki nchini kama mkimbizi wa kisiasa bali anakwenda huko kujipanga zaidi kisiasa. Aidha Lissu pia bado anaendelea na matibabu yake.

 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tundu bovu, Litaendelea kuvuja hata ukitia Gundi na Bazoka ya Bigi jee.

    Sasa, kwa huyu Kibaraka alipataga kama bahati vile kwa mkiti wa saccoz hakumshugulikia katika kinyanganyiro baada ya kulizika na upigaji wa m amlioni ya pesa za matwibwabu yanayo semeka. Saccoz ina mwenye kiti wakudumu panga pangua alikuwaga yumo. sasa tundu asije pwotea akijalibu kutaka uongozi baada ya kuiona disintegration live.

    Tuwndu party news Year.
    Mbweo paid new Year.

    Ati,yule nani pia kauganisha majuu . na ndoaya jinsi amelusiwa. Majuu Wabaya.. Nuksi huli chao Bure.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anaipenda Damu huyu dogo.

      Alihamasisha nchi iingie katika Uvunjifu wa Amani na watu Waingie Balabalani yeye na Genge lake la Ninja tortoise , Watanzania waka m PONDA.

      Akawa hana Jinsi, kaBwaga Manyanga wenzake wanasubiri jalada lao kuanza kusikilizwa , yeye ndio kaludi kula Bwata nna kuku kwa mlija baada ya kukwea pipa Majuu.

      Watanzania tumesha kusoma. Tusikuone tena kwetu.
      Madawa yakizidi mwilini una data. Au dokta anakufanyia makusudi. Alikwambiaga umeponaga na sasa anaendeleaga
      kukutibugi.
      Jameni mbona wanakuchezea, mala mzima mala mgonjwa.

      Delete
  2. Tumepata tetesi, Kwamba, kuna wakili mashuli ambaye aliunganishwa na kupitia Lobati Kiagulanyi amemfugulia jalada la madai kwa kutomlipa ujira wa kumfundisha kampeni bila Sera za kuuza ila fujo kama kwa Jilani zetu wa ngambo ya Mtu Kula.

    Kusua sua kwa intaneti lilikuwa tukio Adhimu kwa Usalama wa nchi yetu na Bando zetu pia zilisalimika.

    Tanzania iko Salama na mungu anadumisha Amani yetu.

    ReplyDelete
  3. Bingwa wa Matusi.
    Bingwa wa Upotoshaji.
    Bingwa wa Ufitinishaji.
    Bingwa wa Usingiziaji.
    Bingwa wa Maigizo na Usanii.
    Bingwa wa Kujifagilia na kuwatema kingenge chake.

    Na kikubwa Zaidi ni BINGWA KUKOSA SERA, UKIWA HUNA SERA
    WABONGO WANA KUFANYA KINYAGO .na ndio lilotokea kinyago oyee

    Ila kkwa Watanzania amegonga mwamba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Mie namuona ka alikuwa Mropokaji Adimu kumshinda Mwalimu salumu. hivyo wako pamoja Ubelijigi.

      Si nasikia huko balafu ya friji inagandisha mpaka Ubongo kama anao. itabidi ........Inasikitisha.

      Delete

Top Post Ad