Mavoko "Ngoma Zangu Zitaongea Siyo Mimi Sipendi Mambo ya Kiki Kama Ule Upande Mwingine"
MKALI wa ngoma za kuyaimba mapenzi kupitia Bongo Fleva, Rich Mavoko amesema kukaa kwake kimya bila kuwa na makeke mitandaoni amefanya makusudi kwa kuwa anahitaji zaidi kazi zake ziongee.


Mavoko ambaye aliwahi kuwa memba wa WCB kabla hajachomoka na kufanya kazi kivyake, alisema kuwa, kujianika
maisha yake binafsi na skendo mtandaoni hayana nafasi kwa sasa katika maisha yake, zaidi anahitaji kuacha mashabiki wake wapate wanachostahili.


Akizungumza na Championi Jumamosi, Mavoko alisema: “Nataka kazi zangu zisikike zaidi uliko kufanya maisha ya uongo hasa ya skendo, hayo mambo kwa sasa hayana nafasi kwangu, naamini kwenye muziki wangu najua nikiongeza kasi kidogo nitafika sehemu ninayoitaka.”


Mavoko alianza mwaka 2020 kwa kuachia mintape ambayo ina nyimbo nane, ambazo kwa kiasi kikubwa zimemsogeza juu, mikwaju kama Bad Boy, Wa Moto, Niwahi na mangoma mengine ambayo yanafanya poa.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments