"Mimi bado sijatumika" - Miss Lucy Charles

 


Miss Mwanza na Mshiriki wa Miss Tanzania 2010 Lucy Charles amefunguka kusema yeye hajatumika sana kwa wanaume ili kupata michongo ya kufanya ishu zingine ambazo zitamuwezesha kwenye maisha.

 

Miss Lucy Charles amesema kuwa jamii inatakiwa kuelewa kwani unaweza ukatumika kwa wanaume na bado usifanikiwe na kupata maendeleo yoyote japo yeye haamini katika hilo.


"Mimi sijatumika lakini siamini kama mtu anaweza akafanikiwa kwa sababu ya kutumika, pia unaweza ukatumika na usifanikiwe jamii inatakiwa ielewe kwani hiyo ni tabia ya mtu, sio lazima uwe staa unaweza ukatumika hata mtu wa kawaida na usipate maendeleo, naamini kwenye kufanya kazi na kutokata tamaa" ameeleza Miss Lucy Charles 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments