Mrithi wa Waziri Mteule Aliyeshindwa Kuapa Apatikana

 


Rais Dkt. John Magufuli, amemteua Prof. Shukrani Manya, kuwa Naibu Waziri wa Madini, Prof. Manya pia ameteuliwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Desemba 11, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kusema kuwa kabla ya uteuzi huo, Profesa Manya alikuwa ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini na uteuzi wake umeanza leo na atapishwa leo mchana.


Profesa Manya, amechukua nafasi ya Francis Ndulane, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa Desemba 9, 2020, na Rais Magufuli, baada ya mteule huyo kushindwa kula kiapo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments