Mtibwa Yaichapa Bao Moja KMCKIKOSI cha Mtibwa Sugar leo Desemba 11 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

 

Bao pekee la ushindi limepachikwa na Salum Kihimbwa dakika ya 21 kwa kichwa akimalizia pasi ya Kanoni aliyamwaga majalo kutoka pembeni mwa uwanja.

 

Licha ya jitihada za KMC kupambana kupitia nyota wao Relliants Lusajo na Emmanuel Mvuyekure kupata bao la kusawazisha milango ilikuwa migumu.

 

Abutwalib Mshery mlinda mlango namba moja wa timu ya Mtibwa amekuwa imara langoni kuokoa hatari zote za vijana wa Kinondoni.

 

Kihimbwa amesema kuwa walipata nafasi nyingi Kwenye mchezo huo ila walishindwa kuzitumia licha ya kupata pointi tatu muhimu.

 

Juma Kaseja, nahodha wa KMC ambaye ni kipa namba moja amesema kuwa makosa ambayo wamefanya yamewaponza.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments