Museven: Sijaona Mtu wa Kuiongoza Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye kwa sasa anawania muhula wa sita madarakani,amesema hajaona mtu mwenye uwezo wa kuongoza Uganda kwa sasa na hivyo ataendelea kuwa madarakani kwa sababu wapiga kura nchini humo bado wanamhitaji kuendelea kuongoza taifa hilo.

 

Akihutubia viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) katika wilaya ya Lukungiri, ambayo ni ngome ya kisiasa ya aliyekuwa mpinzani wake mkuu mara nne Dr. Kiiza Besigye, Museveni amesema kwamba wapinzani wake ni watu wazembe wanaotaka kusukumwa kama mkokoteni.

 

 

Kati ya wapinzani wake 10 katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao 2021, ni waliokuwa makamanda muhimu wakati walipokuwa msituni katika vita vilivyomwezesha kuingia madarakani mwaka 1985.

 

 

Wagombea hao ni Lt. Gen Henry Tumukunde na aliyekuwa kamanda mkuu wa jeshi Maj. Gen. Mugisha Muntu. Museveni amesema kwamba wanaomkosoa walishindwa kazi licha ya kujaribu kila mara kuwaweka katika sehemu tofauti serikalini na sasa ‘wanampigia kelele.’

 

“Wanajua lengo langu katika siasa lakini wanataka kunishawishi niache msimamo wangu. Wanapiga kelele kwamba nastahili kuondoka madarakani utadhani sina pa kwenda,” amesema Museveni akitumia mojawapo ya lugha zinazozungumzwa magharibi mwa Uganda.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pamoja sana Mzee Museveni.

    Kelele zao, Hazina Tija wala Welekeo, nni Vibaraka tu na Wacheza Madogoli.

    Uganda bila Yoweri, ni sawa na mchuzi bila chumvi. Hainogi.

    ReplyDelete

Top Post Ad