Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Muuaji hatari katika historia ya Marekani, Samuel Little afariki DuniaSamuel Little, mtu aliyetajwa na shirika la kijasusi la FBI kama muuaji mkubwa wa kuvizia katika historia ya Marekani amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

Samuel Little, most prolific serial killer in U.S. history, dies

Little alifariki katika hospitali mjini California siku ya Jumatano, idara ya magereza imesema. Alikuwa akihudumia kifungo cha mauaji ya wanawake watatu

Lakini kabla ya kifo chake , alikuwa amekiri kuwauawa wanawake 93 kati ya mwaka 1970 na 2005.

Little aliwalenga watu waliokuwa hawawezi kujitetea, wengi wao wakiwa makahaba ama watumiaji wa mihadarati , walisema maafisa.

Little alikuwa akiuwa bila kuwacha ishara zozote za mauaji, kama vile kuwadunga kisu ama kuwapiga risasi na kwamba mtu huyo alikuwa ameuawa.

Badala yake vifo vyake vingi alivyo uwa vilidaiwa kula dawa kupitia kiasi ama vya ajali na havikuchunguzwa. Baadhi ya miili haijapatikana , kitengo hicho kilisema.

Mwaka uliopita FBI lilisema kwamba wachambuzi wake walisema kwamba madai yote aliokiri kutekeleza yalikuwa ya kweli.

Pia walitoa picha za waathiriwa aliowachora wakati akiwa jela katika jaribio la kuwatafuta aliowaua,Waathiriwa wa Samuel Little

Shirika la FBI lilitoa michoro ya Samuel Little kwa matumaini kwamba waathiriwa watatambulika
Little alikamatwa mwaka 2012 kwa mashtaka ya kutumia mihadarati mjini Kentucky na kusafirishwa hadi California, ambapo maafisa walitafuta vinasaba vyake .

Tayari alikuwa na rekodi mbaya ya uhalifu akiwa na mashtaka ya wizi wa mabavu hadi ubakaji katika maeneo mbalimbali Marekani.

Vinasaba vya DNA vilimuhusisha na mauaji ya watu watatu ambao hayajatatuliwa kutoka 1987 na 1989 katika kaunti ya mji wa Los Angels.

Alikataa kufanya makosa lakini hatimaye alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha , bila fursa ya kuachiliwa katika siku za usoni.

Ramani ya kifo kinachohusishwa na bwana Little kutka kwa data ya FBI
Ramani ya kifo kinachohusishwa na bwana Little kutka kwa data ya FBI

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments