Mwakinyo Abakiza Nyota 2 Kufikia Viwango vya Kina Manny Pacquiao, Agoma Kupigana na Twaha KidukuBondia namba moja nchini, @hassan_mwakinyo_jr kupitia ukurasa wake wa #Twitter amejibu kuhusu kupigana na Bondia mwenzake Mtanzania, #TwahaKiduku.


Ikumbukwe kuwa kupitia viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, boxrec Ijumaa iliyopita, #Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa Super Welter na kuwa na nyota tatu.


Hivyo #Mwakinyo anahitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwamo #MannyPacquiao mwenye nyota tano.


Akijibu swali la Shabiki yake aliyemuuliza kuhusu kumkimbia Bondia Twaha Kiduku, #Mwakinyo alijibu, "Nimebakiza Nyota 2 Kufika Level za kina Manny Pacquiao so kupigana Na Kiduku sidhani kama nitapata izo 2 star zilizobaki Lets focus on internation Levels"

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments