Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwanamuziki Ariana Grande Avalishwa Pete ya Uchumba


Kila mwaka huwa na matukio yake ya kihistoria yanayojiri, mwaka 2020 umeleta makubwa mengi sana bila kusahau COVID-19 na mengineyo lakini yote hayo hayajaweza kusimamisha jambo liitwalo Penzi. Tumeshudia tayari NDOA nyingi za watu maarufu zikifungwa mwaka huu.


Sambamba na hilo, msanii #ArianaGrande kutoka nchini Marekani pamoja na mchumba wake Dalton Gomez ambaye ni mfanyabiashara mkubwa wa Real Estate, wao wamemaliza mwaka kwa kuvishana pete ya uchumba.


Pete hiyo ya #Ariana ainatajwa kuwa imetengenezwa na madini ya Almasi.


Aidha, tovuti ya People inaripoti kwamba wawili hao walianza kuwa kwenye mahusiano tangu mwezi Januari mwaka huu.


Hata hivyo, tangu TMZ kuleta habari hii kivingine mwezi Mei (kwa uthibitisho wa picha za wawili hao wakiwa mgahawani) ndio watu wengi walianza kuelewa uwepo wa penzi jipya mjini. Hilo lilipelekea #Ariana aanze kumpost Bw #Gomez mara kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram.


Ikumbukwe, hii si mara ya kwanza kwa #Ariana kuvalishwa pete ya uchumba, mwaka 2018 pia alivalishwa pete na aliekua mpenzi wake wa kipindi hicho #PeteDavidson na penzi lao likavunjika baada ya mwaka mmoja.


 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments