Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Mwigizaji Taraji P. Henson Afunguka Kutaka Kujia Kipindi cha Janga la Corona


Tatizo la afya ya akili (mental health) sio la kuchukulia poa hata kidogo, mwigizaji Taraji P. Henson amefunguka kwamba alipata mawazo ya kujiua kipindi ambacho alikuwa amejitenga peke yake kwa hofu ya ugonjwa wa Corona.


Kupitia kipindi chake 'Peace of Mind With Taraji' jana Jumatano kupitia ukurasa wake wa Facebook, mwigizaji huyo maarufu alikiri kufikia maamuzi hayo ya kutaka kujitoa uhai wake kutokana na upweke.

-

"Katika kipindi hiki cha janga la Corona imekuwa wakati mgumu sana kwetu sote, na nilipatwa na nyakati za giza. Nilikuwa kwenye eneo lenye kiza kinene, kwa siku kadhaa, sikuweza kunyanyuka kitandani, kitu ambacho kilinifanya kujiona kama sio mimi. Kisha nikaanza kupata fikra za kujimaliza, ilinitokea nyakati mbili za usiku mfululizo." alisema Taraji.


Baada ya fikra hizo alifikia uamuzi wa kununua bastola, na baadaye alianza kumuwaza mtoto wake wa Kiume ataishi vipi? lakini alijiambia kwamba "atasahau tu kwa sababu tayari ni kijana mkubwa." Kilichomsaidia Taraji. P. Henson ni uamuzi wake wa kuanza kuongea na wapendwa wake na kutoa ya moyoni kiasi ambacho ilimsaidia kutokaa na kitu moyoni na kupunguza msukumo wa moyo wake.

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments