Mzee Jengua azikwa na maelfuLeo siku ya Disemba 16, ndiyo ilikuwa safari ya mwisho ya kumpumzisha msanii wa filamu ambaye kwa sasa ni marehemu Mzee Jengua baada ya kufariki dunia siku ya jana Disemba 15 nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwenye picha hapo hilo ndilo jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mzee Jengua, ukisindikizwa na mamia ya watu waliojitokeza kwa ajili ya kwenda kuzika kwenye makaburi ya Mburahati Jijini Dar Es Salaam.

Wachekeshaji na mastaa wa filamu kama Steve Nyerere, Miss Lucy Charles, Mzee Jumbo, Kingwendu, JB, Mama Kanumba, Patrick Kanumba, Bi Staa, Tito, Ringo, Tin White, Kivurande na Hashim Kambi ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye mazishi ya Mzee Jengua.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments