Nahodha AS Vita Awapa Mchongo Yanga FC
KIUNGO wa AS Vita ya DR Congo, Jeremy Mumbere, amesema Yanga itatisha zaidi kama itafanikisha dili la kumsajili mshambuliaji wa DC Motema Pembe, Kadiba kabangu kutokana na uwezo mkubwa alionao mshambuliaji huyo.

 

Yanga imehusishwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mwenye uraia wa DR Congo ambapo yeye mwenyewe alikiri kuwa katika mazungumzo na Yanga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Mumbere ambaye ni Nahodha wa AS Vita, alisema: “Yanga kama watampata Kabangu atawasaidia zaidi kulingana na uzoefu wake wa kucheza ligi mbalimbali na pia kutokana na uwezo mzuri wa kufunga mabao, hivyo kama Yanga watamsajili naamini ataenda kuwaongezea kitu.“

 

Nimemshuhudia Kabangu akicheza na mara kwa mara amekuwa mpinzani wangu tunapokuwa uwanjani, kiukweli ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kufunga kwa usahihi mipira ya vichwa na hata ya chini kwa kutumia miguu, hivyo atawafaa sana Yanga.”

STORI: MARCO MZUMBE | SPOTI XTRA

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments