Nairobi: Aliyekufa na kufufuka sasa afariki kweli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanaume mmoja nchini Kenya aliyedhaniwa amefariki dunia na kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti na “kupata tena fahamu” wiki iliyopita , sasa amefariki kweli, kulingana na vyombo vya habari vya eneo hilo.

Wiki iliyopita, inasemekana kuwa mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti alikuwa anatayarisha mwili wake kuuweka kwenye chumba maalum kwa ajili ya wafu, kabla ya mwanaume huyo kupata fahamu ghafla na kuanza kupiga kelele.

Peter Kigen, 32, ambaye alikuwa ameugua kwa muda mrefu, alipekwa hospitali kupata matibabu na baadaye, akaruhusiwa kwenda nyumbani.

Akizungumza na gazeti la Kenya la Daily Nation, Alhamisi iliyopita, alisema kwamba ni mwenye furaha kuwa hai. “Hii ni kazi ya Mungu,” ameliambia gazeti hilo.

Tukio hilo lilisabisha wengi kutoa maoni yao katika mitandao ya kijamii, na pia likajadiliwa katika bunge la kaunti ya Kericho.

Bunge hilo liliunda timu kuchunguza kile hasa kilichotokea taarifa ambayo iliwaondolea wahudumu wa afya lawama.

Alhamisi, msemaji wa familia alithibitisha kifo cha kweli cha mwanaume huyo kupitia gazeti za Kenya la Standard.

“Kigen alitangazwa kufariki dunia baada ya kufika hospitali ya kaunti ya Kericho alikopelekwa kutoka hospitali ya Kapkatet kwa matibabu zaidi,” Hezbon Tonui amesema.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad