Ndemla Amgaragaza Mukoko wa YangaSAID Ndemla, kiungo wa Simba akiwa amecheza mechi tano kati ya 12 za timu hiyo msimu huu, amehusika kwenye jumla ya mabao manne kati ya 31 huku akiyeyusha dakika 384 akimgaragaza kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe.

 

Mukoko amehusika kwenye mabao matatu kati ya 17 yaliyofungwa na timu yake kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Mwadui uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.Kiungo huyo amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao ndani ya dakika 1,005 ambazo ameziyeyusha uwanjani kwa kuwa alitumia dakika 90 kwenye mechi 11 na dakika 15 kwenye mchezo dhidi ya Prisons.

 

Ndemla amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao, amekuwa na hatari ndani ya uwanja kila baada ya dakika 96, huku Mukoko akiwa na hatari kila baada ya dakika 335.

 

Hizi hapa mechi za Ndemla Simba: Biashara United (81), Gwambina (90), Ruvu Shooting (33), Coastal Union (90) na Polisi Tanzania (90).Mechi za Mukoko ni: Prisons (15), Mbeya City (90), Kagera Sugar (90), Mtibwa Sugar (90), Coastal Union (90), Polisi Tanzania (90), Biashara United (90), Simba (90), Namungo (90), Azam FC (90), JKT Tanzania (90) na Ruvu Shooting (90)

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA,Dar es Salaam

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments