Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ndugai ang’aka sakata la kina Mdee, Chadema

 


Dodoma/Dar. Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alizungumza kwa ukali kuhusu makada 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema, akisema hakubaliani na uamuzi huo aliouita wa mtu mmoja, huku aliyekuwa mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitarajiwa kutoa tamko leo.


Ndugai aliyekuwa akiapisha wabunge wawili walioteuliwa na Rais John Magufuli, alianza hotuba yake kwa sauti ya chini, lakini akaiongeza kadri alivyoendelea kuzungumzia sakata hilo, akieleza bayana kuwa atawalinda wanawake hao.


“Yaani mtu awe na chama, anaburuza anavyotaka yeye? Ndio maana namwambia hawa 19 ni wabunge labda wao wenyewe kwa kutumia utaratibu wa kikatiba; ama wajiuzulu au yatokee yale mambo ambayo yametajwa,” alisema Ndugai.


“Lakini kwa yeye na (katibu mkuu wa Chadema, John) Mnyika wake, wale ni wabunge. Hawawezi wao na genge lao la wanaume wakaweza kuwafanyia hivyo dada zetu”


Alikuwa akizungumzia uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadem,a kuwavua uanachama makada hao 19 kwa kosa la kujitokeza bungeni kuapishwa kinyume na maagizo ya chama hicho na pia kutotii wito wa kwenda mbele ya chombo hicho kujieleza dhidi ya makosa yao.


Chadema, ambayo ilipata mbunge mmoja tu wa majimbo, ilistahili nafasi 19 za ubunge wa viti maalum kulingana na idadi ya kura za ubunge ilizopata, nafasi ambazo Sheria ya Uchaguzi inataka vyama vipendekeze orodha ya majina kulingana na umuhimu wa mtu na kuipeleka Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya uteuzi.


ADVERTISEMENT

Kabla ya wanawake hao kujitokeza Jumanne kwa ajili ya kuapishwa, habari zilisambaa kuwa kulikuwa na mpango huo na Mnyika akasema hajapeleka majina yoyote NEC na kutuhumu kuwepo na njama.


Lakini mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC alimjibu kuwa Tume ilipokea majina hayo kutoka kwa Mnyika, ambaye alikanusha vikali akisema hangeweza kupeleka kabla ya Kamati Kuu ya Chadema kukutana na kupendekeza majina.


Jana, akizungumza baada ya kuwaapisha wabunge wawili walioteuliwa na Rais, Humphrey Polepole na Riziki Lulida, Ndugai aliwaondoa hofu watu wenye wasiwasi kuhusu wanawake hao 19 baada ya chama chao kuwatimua uanachama.


Alisema wabunge wote walioapishwa wataendelea kutambuliwa kuwa ni wabunge kamili ikiwa ni pamoja na 20 wa Chadema, akiwemo wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Aida Khenah.


“Kwa wale waliokuwa na wasiwasi wale wabunge 19 kuna hili kuna lile, niwahakikishie kuwa wale ni wabunge kamili wa Bunge la Jamuhuri ya Tanzania… Nawaomba Watanzania wote tupige vita na tukatae ukandamizaji dhidi ya wanawake katika jamii yetu kwa kisingizio chochote,” alisema.


“Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisimama na kuanza kuwatukana wabunge hao hadharani, jambo ambalo kwa mtu mzima na mwanaume aliyefundwa ni aibu kubwa.”


Hata hiyo, Mbowe alisema wakati akitoa taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwa hakuna anayefurahia uamuzi huo na kwamba wanaufanya kwa masikitiko kwa kuwa wanawake hao wamekuwa katika harakati za chama hicho.


Mbowe alisema pamoja na Kamati Kuu kufikia uamuzi huo, bado wanawake hao wana nafasi ya kukata rufaa Baraza Kuu au kuandika barua ya kuomba radhi.


Na kuhusu uamuzi kuufanya peke yake, Mbowe alisema watu walikuwa wakitaka ajitokeze kuzungumzia suala hilo lakini aliamua kukaa kimya.


“Kama kiongozi mkuu, nikizungumza nazungumza with authority (na mamlaka) baada ya kukutana na Kamati Kuu yangu. Na ndio maana leo nazungumza,” alisema Mbowe Ijumaa usiku.


Lakini Ndugai alisema jana kuwa anachukua nafasi hiyo kumuonya Mbowe na kumkanya asione sifa katika jambo hilo na kwamba wanawake ni mama zao, dada zao na shangazi zao na hivyo wanakosea watafutwe, kukaa nao na kupata maelezo yao na si kuwafukuza kama vibaka.


“Hivi kweli rafiki yangu Freeman Mbowe umesahau Halima alivyovunjika mkono kwa kukufuata magereza, umesahau Ester Bulaya alivyozimia akapelekwa Agha Khan hajitambui kwa ajili yako Mbowe. Umesahau Esther Matiko amelazwa Segerea mara ngapi kwa ajili yako?” alihoji Ndugai.


“Mshahara wao ni kufukuzwa hadharani vile kwa utaratibu usiokuwa wa kiutu bila hata kuwasikiliza? Haiwezekani. Analalamikka mwanachama wake Nusrat (Hanje) alikuwa mahabusu kwanini ameachiwa na kuapishwa kuwa mbunge. Ulitaka afie magereza? Katoka sasa, huyu kiongozi,” alieleza Ndugai.


Alisema hivi karibuni atawapanga wabunge wote kwenye kamati mbalimbali zitakazoundwa baada ya Rais John Magufuli kuunda baraza la mawaziri.


Hali bado inazidi kuwaka ndani ya Chadema baada ya jana kuibuka baraza la wazee wa chama hicho wa mkoa wa Dar es Salaam wakitaka kufanyika uchunguzi wa kina na kuchukuliwa hatua kwa watu waliohusika na mchakato wa kufanikisha makada hao 19 kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalum.


Makada hao ni Halima Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Bawacha, Esther Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.


Wengine ni Asia Mohammed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Flao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.


Macho na masikio sasa yataelekezwa leo katika mkutano wa Mdee, ambaye alivuliwa wadhifa wa Bawacha wakati atakapozungumza na wanahabari kuanzia saa 3:00 asubuhi kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo uamuzi wa kuvuliwa uanachama na nyadhifa zao.

  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

1 Comments

 1. Asante Mh Spika wa bunge la Jamuhuri ya Tanzania kwa kusimamia Haki juu ya Waheshimiwa Wabunge Wateule.

  Nnacho shindwa kumwelewa Flee Mani ni uelewa wake na minyika
  kwamba, Hawa Waheshimiwa Wabunge kina Mama Majasiri ni wakuungwa mkono kwenda kulitumikia Taifa letu kuleta Maendeleo kama walivyo kijenga Chama cha CDM.

  Ni ukweli usio pingika, kuwa kilipofika chama wao wana mchango mkubwa sana.

  Na mazingira aliopelekea huu uamuzi/Azimio batili ni uchakachuaji wa kujitoa Kimasomaso wa Wajumbe Nuksi.

  Gender equality, Haki na Usawa to Empower a Woman is a call of the Day.

  Mbowe, Jitathmini na Utathmini utu wako kama Kiongozi usie na Mshinikiizo katika mihemko, Manyanga uliobwagiwa na yule
  tafakari uchezaji wake kabla ya kupeleka Jahazi Mrama.

  Agwe Muwaha..!! Wampela Viswano. Nene nahulika Viswano.
  SANDENYI SANA, UMLAMSAJE JEMEDALI. MLUNGU AKUTAZ'EE MWAHA..!

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)