Ticker

6/recent/ticker-posts

Ad Code

Ndugai: Kukaa Kijiweni, Kusubiri Ajira za Serikali Mtazamo Hasi
SPIKA Job Ndugai amewataka vijana kuacha fikra potofu ya kusubiri kuajiriwa na serikali, badala yake watumie fursa zilizopo kuibua miradi mbalimbali itakayowainua kiuchumi.

 

Alitoa rai hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa ibada maalumu iliyofanyika kwenye Kanisa la Kristo Mfalme Angalikani, Chamwino, mkoani Dodoma juzi kwa ajili ya kuwahamasisha Watanzania kuzipenda bidhaa zinazozalishwa nchini.

 

“Bado kuna baadhi ya vijana wanaendelea kukaa vijiweni kusubiri nafasi za ajira serikalini, suala ambalo ni mtazamo hasi; hivi sasa kuna fursa nyingi zinazoweza kuwaingizia kipato Ukiwamo ufugaji, kilimo cha zao la zabibu na bustani za mboga badala kuendelea kukaa vijiweni kusubiri kuajiriwa.

 

“Inasikitisha kuona vijana hivi sasa wanashinda vijiweni na majumbani na simu zao kwa ajili ya kuchati, kutafuta ajira na vitu ambavyo havina faida kwao wakati muda huo wangeweza kushughulika na akili ya kuibua miradi mbalimbali ambayo ingewatoa kwenye umaskini,” alisema.

 

Aidha  alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali nchini kuhakikisha vinakuwa na bidhaa zenye ubora ili Watanzania waendelee kujivunia na kuzipenda zaidi bidhaa zao.

 

“Viwanda vikizalisha bidhaa zenye ubora Watanzania watazithamini na kusaidia kukuza uchumi wa nchi na ajira kuongezeka,” alisema.

 

 Tazama Hapa Chini Msanii Rosa Ree Akimkemea Shetani:


  DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL => HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE


Post a comment

0 Comments