Neno ‘negrito’ lamfikisha Edinson Cavani kwa PilatoChama cha soka nchini England FA kimemshitaki mshambuliaji wa Manchester United, Edinson Cavani kufuatia kutumia neno ‘negrito’ mwezi uliyopita lililotafsiriwa kama maneno ya kibaguzi.

Edinson Cavani has been charged by the FA with misconduct following his 'Gracias negrito' Instagram post

Cavani anakabiliwa na matatizo hayo mbele ya FA kufuatia posti aliyoweka nyota huyo akimjibu shabiki kupitia akaunti yake ya kijamii ya Instagram alipoibuka shujaa wa mchezo wao dhidi ya Southampton uliyopigwa Novemba 29 akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja iliyozaa goli kwenye ushindi wa 3 – 2.

Edinson Cavani alikoroga, chini ya uchunguzi mkali

Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 raia wa Uruguay alifuta ujumbe huo na kuomba radhi baada ya kufahamishwa neno hilo la ‘‘Gracias negrito’’ ambalo linatafsirika kwa lugha ya Kiingereza kama ‘Thanks black’ ni la kibaguzi, lakini haikutosha kwa FA kulifumbia macho sakata hilo.

His message translates to 'thanks black' as he appeared to respond to a congratulatory post

Cavani anayo nafasi hadi Januari 4/2021 ya kupinga ama kukubaliana na adhabu atakayopigwa na FA ambayo kwa mujibu wa makosa aina yake atakabiliwa na kifungo cha jumla ya mechi tatu kama atakutwa na hatia.


That Gal ya Rosa Ree Yawa Gumzo Itazame Hapa chini:

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO

Post a comment

0 Comments